1. Utangulizi
·
Nguruwe
ni jamii ya wanyama wasiocheua, na wenye kwato zilizogawanyika.
·
Wanyama
wengine walio kwenye jamii hii ni pamoja na Nguruwe pori na Ngiri
·
Nguruwe
wanafugwa maeneo mengi duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita
·
Nguruwe
ni kati ya mifugo iliyoonyesha ufanisi mkubwa wa kutoa nyama na fedha kwa
kipindi cha muda mfupi na hivyo kufanya kuwa aina ya mfugo anayapependwa kwenye
nchi mbalimbali kwa ajili hasa ya nyama na fedha
2. Faida
za ufugaji wa nguruwe
·
Nguruwe
ni mnyama anayekuwa kwa haraka sana kuliko
baadhi ya mifugo mingine kama: Ng’ombe, Mbuzi
na Kondoo
·
Nguruwe
huzaa na kuongezeka kwa wingi
·
Anauwezo
wa kutumia mabaki yasiyowezekana kwa matumizi mengine
·
Anauwezo
wa kutoa mafuta kwa ajili ya kupika
·
Anauwezo
wa kutengeneza fedha za haraka kwa ajili ya uwezo wake wa kuzaa kwa haraka na
watoto wengi
·
Ni
rahisi kuwalisha nguruwe
·
Wanaweza
kukuzwa kwenye eneo dogo
·
Nyama
yake ni laini na yenye viini lishe vingi
·
Huzalisha
mbolea iliyobora kwa matumizi ya kilimo
3. Aina
za nguruwe
Humu nchini
mwetu kuna kuu tatu za nguruwe
i.
Nguzuwe
wa kienyeji
ii.
Nguruwe
weye asili ya ugenini (Exotic breed)
iii.
Nguruwe
mchanganyiko (crosses): wenye mchanganyiko wa damu ya kienyeji na ugenini (
Local x Exotic) na wenye mchanganyiko wa damu za ugenini (exotic x exotic)
Aina za
Nguruwe (breeds) wenye asili ya ujenini zinazopatikana kwa wingi kwenye
mazingira yetu.
i. Large
white
Sifa
·
Rangi
nyeupe
·
Miili
mikubwa
·
Masikio
yaliyosimama wima
·
Wana
asili ya Uingereza
·
Wanauwezo
wa kuzaa watoto wengi
·
Wana
nyama nzuri
·
Wana
uwezo mzuri wa ukuaji

ii. Landrace
Sifa
·
Rangi
nyeupe
·
Miili
huwa na umbo refu na huonekena wembamba
·
Masikio
yaliyolala na kufunika sehemu ya macho
·
Wanaasili
ya Denmark
·
Ni
wazazi wazuri
·
Ni
wazuri kwa nyama

iii. Saddle
back
Sifa
·
Mwili
wenye rangi nyeusi ulio na mshipi mweupe
unaopitia kwenye mabega
·
Masikio
ya kulala
·
Wana
asili ya Uingereza

NB.
Aina zi za nguruwe zilizotajwa hapa juu wengi wao wamekaa Kwa muda mrefu hivyo kupoteza
nasaba yake kutokana na muingilian wa vizazi mablimbali
4. Mambo
Muhimu ya Kuzingatia utapotaka kuanzisha ufugaji wa Nguruwe
i
Mahitaji
na Matakwa ya soko
§ Ni mahali gani unapotegemea
kuuza mazao yako ya nguruwe/mazao yako yanahitajika wapi?
§ Ni aina gani ya mazao ya nguruwe
yanayohitajika k.m vitoto vya nguruwe, wanaokuwa, walionenepeshwa, au ni
nyama
§ Ni lini zao/mazao fulani ya nguruwe yanahitajika zaidi kwa bei
nzuri
§ Je bei za soko zikoje kwa mazao
mbalimbali ya nguruwe
ii. Aina ya nguruwe utakaofuga: Aina ya nguruwe utakaofuga watategemea
vigezo mbalimbali kama
§ Mahitaji na matakwa ya soko
§ Upatikanaji wa aina za nguruwe
§ Aina ya matunzo unayoweza
kuyahimili
iii. Upatikanaji wa vyakula na bei
zake
§ Aina ya vyakula vinahitajika kwa
makundi mbalimbali ya nguruwe (watoto, nguruwe wanaokuwa, wanaonenepehwa, wenye
mimba, wanaonyonyesha, madume, wenye mimba etc)
§ Upatikanaji wa vyakula katika
eneo na bei zake
iv. Uwepo wa taaluma/uwezo/uzoefu wa
utunzaji wa nguruwe
§ Je unauwezo wa kitaalam au
uzoefu wa ufugaji wa nguruwe?
§ Kama huna, je kuna mtaalam wa mifugo
karibu au mtu mwenye uzoefu dwa wa kukusaidia ?
5. Viwango vya Uwekezaji kwenye ufugaji wa
nguruwe
§ Kati ya mambo yenye garama kubwa
kwenye uwekezaji wa ufugaji wa nguruwe ni mabanda/nyumba, vyakula na ulishaji, Udhibiti
wa magonjwa na garama za ununuzi wa nguruwe.
§ Hata hivyo viwango vya uwekezaji
vinatofautiana kulingana na mfumo wa uzalishaji unaoamua kuutumia.
§ Kwa wastani makisio ya gharama
za uwekezaji zinaweza kutofautiana kama
ifuatavyo
1. Ujenzi wa nyumba/banda 14 %
2. Garama za chakula na ulishaji 70
%
3. Udhibiti wa magonjwa: 4 %
4. Ununuzi wa nguruwe : 10
%
5. Mahitaji mengineyo: 2 %
Jumla 100 %
6. Mifumo ya uzalishaji wa nguruwe
- Uzalishaji mkubwa (Large scale production)
i)
Ufugaji wa ndani (Confinement
rearing):
§ Ufugaji huu nguruwe wanafungwa
ndani ya mabanda yaliyowekewa uzio ambapo nguruwe huwekwa kwa muda wote
§ Mara nyingi wanalishwa vyakula
vilivyotengenezwa na vilivyokamilika kilishe (Compounded balanced rations).
§ Mfumo huu huhitaji kiwango
kikubwa cha uelewa/taaluma ya ufugaji nguruwe
ii)
Ufugaji wa nje (Outdoor rearing):
§ Mfumo huu nguruwe hukuzwa nje
§ Mara nyingi hulishwa majani na
chakula cha ziada cha nafaka
2.
Uzalishaji
mdogomdogo (Small scale production)
i)
Ufugaji
wa ndani
ii)
Ufugaji
wa nje
7. Kuanzisha ufugaji wa nguruwe
Unapoamua kufuga nguruwe ni muhimu kujiuliza
maswali kadhaa, kama:
§ Je kweli una nia ya dhati ya
kufuga nguruwe?
§ Mahitaji na matakwa ya soko,
aina ya nguruwe itakayokufaa, upatikanaji wa chakula na bei zake, utaaluma wa
ufugaji ulionao
§ Mfumo gani wa ufugaji unaofaa
kwenye mazingira na mtaji ulionao?
§ Aina ya nyumba ya nguruwe
inayokufaa na inayokidhi haja ya mazingira uliyonayo?
§ Uanze na nguruwe wangapi na wa
aina gani
§ Je kwa hela nilizo nazo
zinatosheleza kuwafuga nguruwe mpaka nitakapoanza kupata mazao na kuyauza?. Je
kama hazitoshi nitafanyaje?
8. Utunzaji wa Nguruwe
i. Nyumba/makazi ya nguruwe
§ Nyumba ya nguruwe ni kati ya mambo
muhimu kwenye uwekezaji na ufugaji wa nguruwe.
§ Kiasi cha nguruwe unachotaka
kufuga, rika la nguruwe kwa mahitaji mbalimbali na mfumo wa ufugaji wa nguruwe
unaotaka kuufuata ni baadhi ya mambo muhimu yatakayo kuongoza kuamua aina ya
nyumba itakayofaa kuchagua
Sifa
za banda bora
Sakafu:
§ Inashauriwa kuwa na sakafu bora
na imara. Hivyo basi sakafu iliyotengenezwa kwa
saruji na yenye mwinuko (slope), au Mabanzi imara inaweza kutumika
Kuta:
§ Kuta za mabanda ya nguruwe zinatakiwa kuwa imara, ziwe na uwezo wa
kuwasitiri nguruwe wasitoke nje
§ Kuta zinweza kutengenezwa
kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kwa urahisi kwenye eneo unaloishi ili
mradi tu uzingatie uimara na udhibiti wa
nguruwe. Hivyo basi vifaa kama mabanzi, fito
au matofali yanaweza kutumika
Paa:
§ Paa ni muhimu sana kwa nguruwe
ili kumsaidia kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa mfano kumkinga nguruwe na jua
au mvua kwani nguruwe wanauwezo mdogo wa
kustahimili mabadiliko ya hewa kwa sababu ya kutoweza kutoa jasho vilevile mwili wake kuwa na mafuta mengi.
§ Paa liwe na urefu wa kutosha ili
litoe nafasi ya kuingiza hewa ya kutosha ndani ya banda hasa kama
ukuta umezibwa (solid walls)
§ Hivyo basi paa linaweza
kupauliwa vizuri kwa nyasi, makuti, bati n.k
§ Banda lililopauliwa vizuri kwa
nyasi lina uwezo wa kuhifadhi hali nzuri ya hewa ndani ya banda ila haliwezi
kudumu kwa muda mrefu.
§ Paa la bati kama
likipauliwa vibaya halina uwezo wa kuhifadhi mazingira mazuri ya hewa. Lakini
kama likipauliwa vizuri linaweza kuhifadhi mazingira mazuri na kudumu kwa muda
mrefu.
Mfumo wa kuondolea
mkojo na kinyesi
§ Unapotengeneza banda la nguruwe
hakikisha unaweka mfumo mzuri wa kuondoalea mkojo na kinyesi. Vilevile
hakikisha kuwa mkojo na kinyesi hakitapakai ovyo ovyo kwani inaweza kuwa chanzo
cha kueneza magonjwa hasa minyoo.
9. Utafutaji wa nguruwe/Ununuzi wa nguruwe
§ Mambo muhimu ya kuzingatia
wakati wa kutafuta/kununua nguruwe kwa
ajili ya ufugaji ni
§ Lengo la ufugaji ambalo
litakusaidia kubaini aina ya nguruwe watakaofaa
§ Ni vyema kununua nguruwe toka
kwenye shamba au mfugaji mwenye sifa ya kuwa na nguruwe wazuri, na amablo
halina taarifa mbaya ya magonjwa n.k
§ Tafuta taarifa na ikiwezekana
fanya ukaguzi wa shamba unalotaka kununua nguruwe
10 Huduma na matunzo ya makundi mbalimbali ya
nguruwe
Huduma na matunzo
ya watoto wa nguruwe
1. Huduma na matunzo kwa nguruwe anayekaribia
kuzaa
Matayarisho ya chumba cha kuzalia
·
Hakikisha
kuwa chumba cha kuzalia kina nafasi ya kutosha
·
Fanya
marekebisho na ukarabati muhimu kama vile kukarabati
sehemu zilizobomoka au sehemu kuukuu
·
Usiache
sehemu kwenye chumba hicho zitakazoruhusu watoto vya nguruwe kutoka nje ya
banda
·
Hakikisha
mazingira ya ndani ya banda ni masafi.
·
Tenga
sehemu ndogo ndani ya banda kwa ajili ya watoto kujihifadhi
·
Hakikisha
kuwa hiyo sehemu inaweza kutoa hifadhi
ya watoto dhidi ya baridi
·
Unaweza
kuweka matandiko (beddings) kama majani
makavu, maranda n.k ili kujenga mazingira ya joto kwa ajili ya watoto
·
Kama
mama nguruwe alikuwa akikaa kwenye banda jingine ambalo halikuwa maalum kwa
ajili ya kuzalia, utahitajika kumweka kwenye banda hili wiki moja kabla ya
kuzaa
2. Wakati wa kuzaa
·
Wakati
wa nguruwe kuzaa usisumbue zoezi la kuzaa kama mchakato unaendelea vizuri.
Unachotakiwa kukifanya ni kusimamia na
utoe msaada kwa mama nguruwe tu kama kuna
tatizo
·
Baada
ya kuzaa usiwatenge watoto na mama yao
·
Kata
vitovu vya watoto kiasi cha sentimita 3 hadi 5 kwa wembe mpya au kikatio
kilicho safi na
kilichochemshwa
·
Paka
madini ya joto ( tincture of iodine) kitovuni
·
Hakikisha
watoto wote waliozaliwa wananyonya kwa mama yao maziwa ya mwanzo (colostrum)
·
Wasaidie
watoto wadhaifu waweze kunyonya
3. Huduma nyinginezo baada ya kuzaliwa
§ Wapatie watoto madini ya chuma
ndani ya wiki ya kwanza ya kuzaliwa hasa siku ya tatu ya kuzaliwa. Hii ni
muhimu kwa sababu madini ya chuma ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza damu. Lakini
maziwa ya mama nguruwe yana upungufu mkubwa wa madini ya chuma, vilevile watoto
huzaliwa wakiwa na kiwango kidogo sana
cha madini haya. Kutompa madini ya chuma kutaathiri ukuaji, ustahimilifu
magonjwa na hatimaye kusababisha vifo
§ Kata meno yaliyochongoka ya
watoto, hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kumuumiza mama wakati wa kunyonyesha,
vivile, kutoumizana wenyewe
§ Hasi hasa vidume ambvyo
hutavihitaji kwa matumizi ya uzazi. Njia ya kuhasi inayotumika kwa watoto ni
ile ya wazi (open method), wasiliana na mtaalam wa mifugo ili akusaidie kwenye
shoghuli hii
§ Kuweka alama za utambuzi (identification).
Unaweza kutumia njia ya kukata pembezoni mwa sikio (ear notching), au kuvika
vitambulisho maalum kwenye sikio (ear tagging)
4. Kuwapatia watoto chakula maalum (creep
feed)
§ Hiki ni chakula kigumu chenye
mchanganyiko kamilifu wa viinilishe na wanachopewa watoto wa nguruwe wakiwa na
umri wa wiki ya pili hadi wiki tatu
§ mahitaji ya watoto kipindi hiki
ni makubwa kulinganisha na uwezo wa maziwa wanayonyonya kutosheleza mahitaji
hayo
§ Hii itawasaidia watoto kuzoea
chakula kigumu, kutosheleza mahitaji yao
ya viini lishe, na hivyo huwawezesha watoto kukua kwa haraka
i
Kuwaachisha watoto kunyonya
§ Hili ni zoezi la kuwatenganisha
watoto na mama yao
§ Zoezi hili halitakiwi kufanywa
kwa ghafla. Fanya taratibu na kwa makini ili kutowapa watoto mshituko
§ Wanatakiwa wazoeshwe kula
vyakula vigumu taratibu kabla ya kuachishwa kama
ilivyoelekezwa hapo juu
§ Watoto wanatakiwa waachishwe
kunyonya kwa kuzingatia uzito wao na sio umri wao
§ Ni vyema kuwaachisha watoto kunyonya
wakiwa na uzito wa kilo 9 – 11
§ Kama watoto wamelelewa vizuri watafikia
uzito huo wakiwa na umri wa siku 58 (Takriban miezi miwili)
§ Kama watoto watakuwa na uzito chini
ya kilo 9 kwenye umri wa miezi miwili inaashiria kuwa walipatiwa matunzo duni
§ Baada ya kuwaachisha watoto
kunyonya wanatakiwa kupatiwa mahali pazuri pa kukaa, penye nafasi ya kutosha,
na kuwe na vyombo vya chakula na maji
§ Usiweke kundi kubwa la watoto
(mfano zaidi ya watoto watatu) uliowaachisha kunyonya kwenye banda moja. Ni
vyema watengwe kati ya majike na vidume
§ Watoto uliowaachisha wanatakiwa kulishwa
chakula kidogokidogo lakini kwa mara nyingi
VYAKULA VYA NGURUWE NA ULISHAJI
A. Utangulizi
Lishe ya nguruwe ni moja
ya swala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe.
Lishe inagarimu yapata asilimia sabini
na hata zaidi ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi
yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na
lishe duni. Lakini kama nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa
uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.
B. Faida za kulisha lishe bora kwa nguruwe
1. Lishe bora
huharakisha ukuaji wa nguruwe na kupata uzito unaohitajika kwa kipindi kifupi.
2. Lishe bora
hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji sababu nguruwe
atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito
mkubwa
3. Lishe bora
itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora
huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na mama nguruwe na hivyo kuongeza
idadi ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda
C. Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe
Chakula cha nguruwe
kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni
1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini(Wanga)
k.m
§
Pumba
za mchele, Pumba za mahindi, Pumba za ngano, Machicha ya pombe yaliyokaushwa, Mihogo, Viazi vitamu,
viazi mviringo, miwa, Ndizi mbichi, zilizoiva au zilizopikwa na makombo ya
vyakula vya viasili vya wanga n.k.
2. Vyakula vya kujenga mwili (Protini) k.m
§ Mashudu ya
alizeti, mashudu ya pamba na mawese, unga wa dagaa/samaki, damu iliyokaushwa
3. Vyakula vya asili ya madini
§
Chumvi ya mezani, chokaa ya mifugo (Limestone),
mifupa iliyosagwa (bone meal), madini maalum ya nguruwe (Pig mix), madini
mchanganyiko (k.m. maklic), madini ya chuma (hasa kwa watoto wa nguruwe) n.k.
4. Vyakula vya asili ya vitamini k.m
§ Majani mabichi
laini, Mbogamboga, Matunda k.m parachichi,
maembe, mapapai n.k, viungo mboga kama nyanya, bilinganya n.k.
Michanganyiko maalumu yenye viasilia vya vitamini k.m. Vitamini premix n.k.
*5. Maji
§ Hii ni lishe
muhimu kwenye chakula cha nguruwe, ila tofauti na viini lishe vingine
vilovyotajwa hapo juu ambapo nguruwe anapewa kwa vipindi/muda na kiwango
maalum, maji yanahitajika kwa nguruwe muda wote.
D. Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe
Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:
·
Mchanganyiko wako uwe na viinilishe vinne
vilivyotajwa hapo mwanzo
·
Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana
kwa urahisi na bei nafuu kwenye mazingira yako
Mfano jedwali Na 1
linaonyesha michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.Viinilishe
vilivyoonyeshwa vinapatikana kwa wingi nyanda za juu kusini hivyo vyakula
vilivyoonyeshwa vinawezwa kutengenezwa kwenye ngazi za kaya.
- Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa wafugaji walioko kwenye mazingira ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
- Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga machicha ya pombe na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi.
- Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga na mashudu ya mawese yanapatikana kwa urahisi.
- Mchanganyiko namba 4: kwa wale ambao pumba za mpunga na mahindi yanapatikana kwa urahisi.
- Mchanganyiko namba 5: kwa wale ambao soya inapatikana kwa urahisi.
E. Kiasi na namna ya kulisha
·
Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula
mara mbili (asubuhi na mchana) au zaidi kwa siku
·
Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na
rika tofauti kimeonyehwa kwenye gedwali Na 2
·
Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji
wanashauriwa kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya kijadi kama vyakula vya ziada
mfano, majani mabichi laini, majani ya maboga, mbogamboga, matunda kama
maparachichi, majani ya viazi n.k.
JEDWALI Na 1: MICHANGANYIKO MBALIMBALI YA CHAKULA CHA NGURUWE (growers and finishers)
N |
Aina ya viini lishe |
Michanganyiko Mbalimbali( uzito wa kilo 100) |
||||
1 |
2 |
3 |
4 |
5 |
||
1 |
Vyakula vya wanga |
|
|
|
|
|
1. Pumba za mahindi |
70.25 |
32 |
43.00 |
30.00 |
48.00 |
|
2. Pumba laini za mpunga |
- |
25 |
25.00 |
33.00 |
28.75 |
|
3. Machicha ya pombeyaliyokaushwa |
- |
21 |
- |
- |
- |
|
4. Mahindi yaliyobarazwa |
- |
- |
- |
10.00 |
- |
|
2 |
Vyakula vya protini |
|
|
|
|
|
A. Protini ya nafaka |
|
|
|
|
|
|
1. Mashudu ya alizeti |
22.00 |
14 |
14.25 |
22.00 |
9.00 |
|
2.Mashudu ya michikichi |
- |
- |
10.00 |
|
- |
|
3. Soya iliyochemswa na kubarazwa |
- |
- |
- |
- |
10.00 |
|
B. Protini ya Wanyama |
|
|
|
|
|
|
4.Unga wa dagaa/samaki |
4.00 |
2.00 |
4.00 |
3.25 |
1.00 |
|
5.Damu iliyokaushwa |
- |
2.25 |
- |
- |
- |
|
3 |
Vyakula viasili vya madini |
|
|
|
|
|
|
|
1. Chumvi ya mezani |
0.50 |
0.50 |
0.50 |
0.50 |
0.50 |
|
|
2. Chokaa ya mifugo |
2.00 |
2.00 |
1.00 |
2.00 |
2.5 |
|
|
3. Unga wa mifupa |
1.00 |
1.00 |
2.00 |
1.00 |
- |
|
|
4. Madini na vitaminimchanganyiko |
0.25 |
0.25 |
0.25 |
0.25 |
0.25 |
|
|
Jumla |
100. |
100 |
100. |
100. |
100.00 |
Jedwali na 2: Viwango vya kulisha nguruwe wa uzito mbalimbali
|
Na
|
Wakati
|
Uzito wa nguruwe (kg)
|
kiasi cha chakula
(kilo kwa siku)
|
|
1.
|
Baada
ya kuachishwa kunyonya hadi uzito kiasi
|
10 - 17
|
0.75
|
|
2.
|
Uzito
uliozidi kiasi kidogo
|
18 - 29
|
1.00
|
|
3.
|
Uzito
wa kawaida
|
30 - 40
|
1.50
|
|
4.
|
Uzito
mkubwa kiasi
|
41 - 60
|
2.00
|
|
5.
|
Uzito
mkubwa
|
61 - 80
|
2.5
|
|
6.
|
Uzito
mkubwa sana
|
81 -
100
|
3.00
|
MIFUMO WA ULISHAJI: Vipindi na madaraja mbalimbali
1.
Kipindi
cha mimba kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha
A. Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa
·
Apatiwe
chakula kiasi k.m. kilo mbili kwa siku
·
Kiasi
hiki kiendelee hadi wiki 3 kabla ya kuzaa
B. Wiki tatu kabla ya kuzaa
·
Ongeza
chakula kufikia kilo 2½.
C. Wiki moja kabla ya kuzaa
·
Anza
kuopunguza chakula taratibu hasa vyakula vya nafaka (Concentrate rations).
·
Ongeza
vyakula vya mbogamboga, majani laini na
matunda (laxative meals.
D. Siku ya kuzaa
·
Usimpe
chakula chochote cha nafaka.
·
Mpe
vyakula vya mbogamboga vilaini kiasi kidogo tu
·
Mpatie
maji ya kutosha.
E.
Siku
ya 1 – 2 baada ya kuzaa
·
Mpe
½ kilo ya chakula kamilifu.
F.
Siku
ya 3 na kuendelea
·
Ongeza
chakula cha nafaka kwa kiasi cha kilo 1 kwa siku.
·
Ongeza
kufikia kiwango kinachohitajika kulingana na idadi ya watoto alionao mama
nguruwe.
Zingatia
·
Mama
nguruwe anahitaji kilo 3 za chakula kwa matumizi yake ya kawaida.
·
Atahitaji
kiasi cha theluthi moja (1/3)
ya kilo ya chakula kwa kila mtoto aliyenae
Mfano: kama mama ana watoto 9 atahitaji kiasi gani cha chakula?
|
Mahitaji
mama peke yake
|
Mahitaji
kutokana na watoto
|
Kiasi cha chakula kwa siku
|
|
3kg
|
Theluthi moja x 9
|
Kilo
6 kwa siku
|
3 + (1/3 x
9) = 6 Kg
·
Endelea
kumpa kiwango hicho cha chakula mpaka ifikapo wiki moja kabla ya kuwaachisha
watoto kunyonya.
·
Wiki
moja kabla ya kuwachisha punguza kiwango taratibu mpaka kufikia kilo 3½ kwa
siku.
G. Baada ya kuachisha kunyonya
·
Mama
nguruwe wapatiwe chakula bora kilicho na kiwango kikubwa cha madini
na vitamini kiwango cha kilo 2 –
3 kwa siku.
·
Hii
itamsaidia kuivisha mayai, hivyo kumsaidia kupata joto mapema.
·
Ikiwa
hivyo basi siki ya nne hadi tano atapata joto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni